Nafasi ya Utulivu kwa Mwanamke Na Mchg. Joash Aila
Mtoaaji wa mafafanuzi na mwandishi wa kitabu hiki ni Mchungaji Joash Aila ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa Kaniza la Kinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kariakoo. Mwenye shahada mbili za elimu ya Juu ya Theologia kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira na Shahada ya Sanaa ya Muziki wa Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini makumira naatumaini kitabu hiki kitatusaidia.
Kitabu hiki kimekusudiwa kumsaidia mwanamke katika kutambua thamani ya nafasi yake katika jamii na hivyo kuwa tayari kuilinda wakati wote.
Maisha ya mwanamke yanatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, jamii moja hadi nyingine, kabila moja hadi jingine na kutoka katika familia moja hadi nyingine.
Kutokana na kuwepo kwa utandawazi, wasichana wengi pasipo kuchunguza wamejiingiza kwenye kuonekana kituko katika jamii ya Kitanzania na kupoteza nafasi yao kama maandiko yananyosema.
| Seller | REVJOASHAILA |
|---|---|
| Author | Mchg. Joash Aila |
| Good Read | Yes |
| Total Pages | 63 |
| Publisher | - |